Yanga yapiga hodi Singida Bs kumtaka Frank Assink


 Klabu ya Yanga SC imeanza rasmi mazungumzo na Singida Black Stars kwa lengo la kumsajili beki wa kati raia wa Ghana, Frank Assink, kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza Septemba 16.

Taarifa kutoka ndani ya klabu zinaeleza kuwa Yanga inataka kuimarisha safu ya ulinzi kwa kuongeza beki wa kati wa kigeni mwenye uwezo wa juu, na Assink aliyeonyesha kiwango cha kuvutia msimu uliopita akiwa na Singida BS, anaonekana kuwa chaguo bora kwa kikosi cha kocha Romain Folz

Endapo dili hili litakamilika, Yanga italazimika kuondoa jina la mchezaji mmoja wa kigeni katika usajili wake ili kumpisha Assink.

Miongoni mwa wanaoweza kuathiriwa na hatua hiyo ni Yao Kouassi, ambaye licha ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja, huenda asijumuishwe katika usajili wa awali hadi pale atakapoimarika, na pengine kurejeshwa katika dirisha dogo la usajili.

Yanga kwa sasa inaendelea na maandalizi makali kuelekea msimu mpya, ikilenga sio tu kutetea mataji ya ndani, bali pia kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa.

Usikose kuitazama mechi za michuano ya CHAN na LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA kudownload app

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post