Sakata la usajili wa mshambuliaji wa Yanga SC, Clement Mzize, limegeuka kuwa gumzo kubwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Lakini ukifuatilia kwa umakini, utagundua kuwa wachambuzi wanaolivalia njuga zaidi suala hili ni wale wale ambao mara nyingi wamekuwa mstari wa mbele kuikosoa Yanga kwenye mambo mbalimbali.
Swali kubwa linabaki: Kwa nini Mzize? Na si wachezaji wengine waliopokea ofa kubwa kutoka nje?
Mfano rahisi ni wakati Yanga ilipopokea ofa kwa ajili ya kiungo wake nyota Stephane Aziz Ki, hakukuwa na mijadala mikubwa ya aina hii. Lakini kwa Mzize, kila kona imejaa mjadala, presha na mijadala ya moto.
Nini Kiko Nyuma ya Sakata Hili?
Kuna mambo matatu yanayoweza kuwa kiini cha shinikizo hili:
Wakala na wachambuzi “wanaotumika”
Inawezekana wasimamizi wa Mzize wanashirikiana na baadhi ya wachambuzi maarufu kupeleka shinikizo kwa Yanga ili wakubali ofa wanayoitaka wao ambayo itawanufaisha zaidi binafsi kuliko klabu. Hii inaweza kueleza kwa nini ofa yenye thamani kubwa (dola 900,000) imepuuzwa kwa kushinikiza ofa ndogo (dola 600,000).
2. Kupunguza nguvu za Yanga kimashindano
Mzize kwa sasa ni mmoja wa washambuliaji hatari zaidi kwenye Ligi Kuu Bara. Kumuondoa Yanga sasa kunamaanisha kupunguza silaha kubwa ya kikosi, jambo ambalo litawapa ahueni wapinzani, wakiwemo watani wa jadi, Simba SC.
Mpango wa “njia ya panya” kumpeleka Msimbazi
Kuna hofu isiyo rasmi kwamba kama Yanga watakubali ofa ya moja ya timu zinazopendekezwa na wakala wake, huenda akajikuta akicheza Simba SC baada ya muda mfupi. Historia ya usajili kati ya timu hizi mbili imejaa mikwaruzano ya aina hii, Simba ikijaribu kulipa kisasi kwa Yanga baada ya kupokonywa nyota wao muhimu kama Mohammed Hussein Zimbwe Jr, na kufeli kwa majaribio ya kuwasajili Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli na Mudathir Yahya.
3. Mpango wa “njia ya panya” kumpeleka Msimbazi
Kuna hofu isiyo rasmi kwamba kama Yanga watakubali ofa ya moja ya timu zinazopendekezwa na wakala wake, huenda akajikuta akicheza Simba SC baada ya muda mfupi. Historia ya usajili kati ya timu hizi mbili imejaa mikwaruzano ya aina hii, Simba ikijaribu kulipa kisasi kwa Yanga baada ya kupokonywa nyota wao muhimu kama Mohammed Hussein Zimbwe Jr, na kufeli kwa majaribio ya kuwasajili Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli na Mudathir Yahya.
Hata zaidi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ali, kupitia Instagram, alionekana “kuishauri” Yanga kumuuza Mzize, jambo lililotafsiriwa na mashabiki kama jaribio la kisiasa ndani ya soka.
Mchezo Uliopo
Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, mabosi wa Yanga wameshtukia mchezo wa nyuma ya pazia. Swali kubwa ni: Kwa nini wakubali dola 600,000 wakati mezani kuna dola 900,000?
Hofu ni kwamba kuna klabu inaweza kumnunua Mzize kwa fedha kidogo, kisha baada ya muda mfupi akatangazwa kutolewa kwa mkopo Simba SC
Kwa sasa, Yanga imeweka msimamo wa “hakuna mauzo kwa mashinikizo” na inaonekana wako tayari kumbakisha Mzize kama hawatapokea ofa inayokidhi tathmini yao, hata kama hiyo inamaanisha kukosa fedha ili kulinda maslahi ya klabu na kuepuka hila za wapinzani.
Usikose kuitazama mechi za michuano ya CHAN na LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA kudownload app

Post a Comment