Klabu ya Bandari Fc ya Kenya inatajwa kualikwa na Yanga kwenye Tamasha la Wiki ya Mwananchi ambalo kilele chake itakuwa Septemba 12 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Tukio la Wiki ya Mwananchi litahusisha burudani na litahitimishwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ambayo itaalikwa
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amekiri kumekuwa na ugumu kupata timu nje ya Afrika Mashiriki kutokana na muingiliano wa ratiba
Nchi nyingi Afrika ligi zao tayari zimeshaanza isipokuwa Afrika Mashariki ambako michuano ya CHAN inaendelea ikitarajiwa kufika tamati August 30
Bandari Fc iliyomaliza nafasi ya nane katika ligi kuu ya Kenya msimu uliopita, huenda ikapata fursa hiyo ya mualiko
Ikumbukwe pia Wiki ya Mwananchi itafanyika siku nne kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao utapigwa Septemba 16, hivyo mchezo dhidi ya Bandari utakuwa wa burudani zaidi na pengine kocha Romain Folz atalazimika kupumzisha silaha zake muhimu kuelekea mchezo dhidi ya Simba
Usikose kuitazama mechi za michuano ya CHAN na LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA au HAPA kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.
.jpeg)
Post a Comment