JONAS MKUDE NA JOHN BOCCO KUAGWA SIMBA DAY


 Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ali amesema manahodha wa zamani wa Simba John Bocco na Jonas Mkude wamealikwa katika Tamasha la Simba Day litakalofnyika Septemba 10

Ahmed amesema Simba inathamini mchango wa wachezaji hao na huu ndio wakati sahihi wa kuwaaga baada ya utumishi wao wa muda mrefu

"Siku ya Simba ni nafasi kubwa ya kuwapa heshima watu waliofanya makubwa ndani ya Simba , tunatambua , tunakumbuka na tunathamini mchango wao"

"Mwaka huu kwenye Simba Day tutawaalika wachezaji wetu wawili wa zamani ambao wamefanya makubwa ndani ya Simba yetu”

“Nahodha wetu wa zamani ambaye amedunu Simba kwa miaka 6 , ambaye ametupa makombe 4 na ametupeleka Robo Fainali mara 4 , kwa sasa amestaafu rasmi soka hivyo ni nafasi ya sisi kumpa shukran John Rapahael Bocco”

“Lakini siku hiyo hiyo tutaenda kumuaga nahodha wetu mwingine aliyeitumikia Simba kwa miaka 15 , ameondoka mwaka juzi lakini hatukupata nafasi ya kumuaga. Hii ni fursa ya kipekee kwetu kumuaga kipenzi chetu Jonas Mkude,” alisema Ahmed

Usikose kuitazama mechi za michuano ya CHAN na LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu mapema itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA au HAPA kudownload app kumbuka app bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama Apk ikileta neno harmful usiogope.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post