NABY CAMARA ATAMBULISHWA MSIMBAZI

 


Kiungo wa Kimataifa wa Guinea Naby Camara (23) amejiunga na Simba baada ya wiki moja ya kujifua na Wekundu hao wa Msimbazi huko Misri

Kiungo huyo wa zamani wa klabu ya CS Sfaxien, amesaini mkataba wa miaka miwili. Anatua Simba akitokea klabu ya Al Waab Fc ya Qatar ambayo aliitumikia kwa msimu mmoja na nusu akitokea Sfaxien

Camara anamudu kucheza nafasi ya kiungo mkabaji na beki wa upande wa kushoto

Inaelezwa Mkufunzi wa Simba Fadlu Davids ameidhinisha usajili wake baada ya kuvutiwa na uwezo wake hasa alipotumika kama mlinzi wa kushoto

Usajili wake umefuta mpango wa Simba kumsajili Mcongomani Hernest Malonga ambaye nae alikuwa na kikosi cha Simba huko Ismailia

Usikose kuitazama mechi ya RAYON SPORT VS YANGA IJUMAA HII pia michuano ya CHAN na LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA kudownload app ikileta neno its harmful usiogop ni kwasababu bado hatujaiweka playstore ni APK

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post