Ally Kamwe afunguka haya mapokezi ya Yanga leo nchini Rwanda


 Yanga tayari iko Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports ambao utapigwa kesho Ijumaa katika uwanja wa Amahoro. Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Tanzania Romain Folz

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema licha ya muda mfupi ambao kocha huo amepata kukiandaa kikosi, wachezaji wako tayari kupambana na kuwapa furaha mashabiki wao

Kamwe amesema Yanga imepata mapokezi makubwa Kigali ambayo yamemshangaza Folz na baadhi ya wachezaji wapya waliojiunga na timu hiyo katika dirisha hili

"Timu ilipowasili uwanja wa ndege tulipata mapokezi makubwa ambayo yalimshangaza kocha wetu Romain Folz na hata nyota wapya. Mapokezi haya ulikuwa ujumbe mahsusi kwao kuwaonyesha Yanga ni kubwa kiasi gani"

"Naweza kusema kazi kubwa iliyofanyika katika maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Rayon ilikuwa kujenga utimamu wa mwili. Maandalizi ya kimbinu yalifanyika kwa asilimia 25. Lakini wachezaji wetu wako tayari kupambana na kuwapa furaha mashabiki wetu hapa Rwanda na huko nyumbani Tanzania," alisema Kamwe

Akizungumzia mipango ya pre-season baada ya mchezo huo, Kamwe amesema kikosi cha Yanga kitarejea jijini Dar es salaam kukamilisha maandalizi yake

"Mpaka sasa sijapewa taarifa kama timu itasafiri nje ya nchi kuendelea na pre-season hivyo baada ya mchezo dhidi ya Rayon tutarejea nyumbani (Tanzania) kuendelea na maandalizi yetu," aliongeza Kamwe

Awali kulikuwa tetesi kuwa Yanga ingesafiri nje ya nchi kukamilisha wiki mbili nyingine za pre-season. Lakini ni wazi kwa muda uliobaki, uamuzi wa kukamilisha pre-season Tanzania ni bora zaidi

Usikose kuitazama mechi ya RAYON SPORT VS YANGA IJUMAA HII pia michuano ya CHAN na LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA kudownload app ikileta neno its harmful usiogop ni kwasababu bado hatujaiweka playstore ni APK

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post