Kwa mujibu wa mashuhuda, ng’ombe huyo, anayemilikiwa na Bwana Emmanuel Mwita, alikuwa akionekana mwenye uchovu na kuhema kupita kiasi kwa siku mbili mfululizo, hali iliyomlazimu mmiliki kumuita mkunga wa wanyama wa kijijini humo.
Lakini wakati wa uchungu, tukio hilo liligeuka kuwa jambo la kutisha baada ya kichwa cha ajabu kuonekana kikitoka, kikiwa na macho mawili makubwa, pua pana na mdomo unaofanana na wa binadamu.
Mara baada ya tukio hilo, uvumi ulisambaa haraka kwamba kuna nguvu zisizo za kawaida zinahusika, baadhi ya wakazi wakihusisha tukio hilo na vitendo vya kishirikina vilivyowahi kuripotiwa katika maeneo jirani, huku wengine wakiamini kuwa ni ishara ya laana au mikosi.
Polisi wa eneo hilo walifika haraka na kuamuru kwamba mzoga wa ndama huyo uchunguzwe na wataalamu wa mifugo kabla ya kuzikwa ili kuepuka maambukizi ya maradhi yasiyojulikana. Soma zaidi hapa

Post a Comment