Joseph alikuwa kijana mwenye nguvu na mipango mikubwa ya maisha. Alikuwa ameoa na alikuwa na watoto wawili wadogo ambao walimtegemea kwa kila kitu.
Alifanya kazi kama mwalimu wa sekondari katika kaunti ya Kisii, na kila mtu kijijini alimwona kama mfano wa kuigwa. Lakini maisha yake yalibadilika ghafla alipogunduliwa kuwa na ugonjwa wa kansa ya koo.
Dalili za kwanza zilikuwa ndogo; sauti yake ilianza kudhoofika na akawa na maumivu ya koo yasiyoisha. Alipokwenda hospitalini, alipewa dawa za kawaida lakini hali haikuboreka.
Vipimo vya kina vilipofanywa vilithibitisha kwamba alikuwa na saratani. Habari hiyo iliwavunja moyo wote, mkewe akilia mchana kutwa na watoto wake wakibaki wakishangaa kwanini baba yao hakuwa na furaha tena. Soma zaidi hapa

Post a Comment