Ilikuwa siku ya kawaida ya jioni pale Moi Avenue, Nairobi. Watu walikuwa wakiharakisha safari zao za kurejea nyumbani, wengine wakiendesha biashara zao za mitaani.
Miongoni mwa umati huo alikuwepo Kevin, kijana aliyekuwa akifanya vibarua vya hapa na pale. Hakujulikana sana – alikuwa mmoja wa wale vijana ambao kila siku hupita mitaani wakitafuta fursa yoyote ya kujipatia mkate wa kila siku.
Lakini siku hiyo kulikuwa na tukio lililogeuza maisha yake milele. Kevin alipokota karatasi ndogo iliyokuwa imetupwa karibu na duka moja la jumla.
Wengi walipita bila kuiona, lakini macho yake yalivutwa nayo. Alipoifungua, aligundua haikuwa karatasi ya kawaida – ilikuwa ni barua ya kazi iliyokuwa imetelekezwa, ikionyesha tangazo la nafasi wazi katika kampuni kubwa ya kimataifa yenye ofisi zake Nairobi. Soma zaidi hapa

Post a Comment