Yanga kushusha mkurugenzi wa Ufundi kutoka South Africa


 Klabu ya Yanga inatarajiwa kumtangaza Paul Matthews kuwa Mkurugenzi wa ufundi akichukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Abdihamid Moallin ambaye alibadilishiwa majukumu na kuwa Kocha Msaidizi

Matthews alikuwa Mkurugenzi wa ufundi katika klabu ya SuperSport United, alijiuzulu nafasi yake baada ya timu hiyo kuuzwa na sasa ikifahamika kama Siwelele Fc

Matthews alikuwa sehemu muhimu katika usajili wa wachezaji wa timu hiyo, na alipewa sifa kwa usajili wa wachezaji kama Teboho Mokoena alipovutwa kujiunga na klabu hiyo kutoka Harmony Academy, pamoja na Sipho Mbule.

Ime Okon alikuwa mmoja wa vipaji vipya vilivyogunduliwa na Matthews, ambaye alikuwa na majukumu mengi katika Matsatsantsa, yakiwemo ya kusaka vipaji, usajili, na uchambuzi wa utendaji.

Wakati akiwa Tuks, wachezaji kama Andile Jali, Bongani Khumalo, Grant Kekana, Bongani Zungu, na Buhle Mkhwanazi walijiunga na kikosi hicho, ambapo alikuwa kocha msaidizi na mkuu wa usajili kwa kipindi cha miaka saba

Akiwa ni mtu anayeheshimika katika soka la Afrika Kusini, anamiliki leseni ya UEFA B, akiwa amewahi kufanya kazi na AmaTuks, Jomo Cosmos, na Tembisa Classic.

Wakati akiwa Tuks, wachezaji kama Andile Jali, Bongani Khumalo, Grant Kekana, Bongani Zungu, na Buhle Mkhwanazi walijiunga na kikosi hicho, ambapo alikuwa kocha msaidizi na mkuu wa usajili kwa kipindi cha miaka saba

Matthew sasa anajiunga na benchi la ufundi la Yanga pamoja na Kocha Mkuu Romain Folz, katika nafasi ya Mkurugenzi wa Ufundi.

Vyanzo vimedhibitisha kuwa anatarajiwa kuwasili Tanzania leo Ijumaa, kuanza enzi mpya na Wananchi ambao walifunga msimu uliopita kibabe kwa kushinda mataji matano 

Usikose kuitazama mechi ya YANGA VS SAFARI LAGER CUP LIVE bure kupitia simu yako download App yetu kutazama mechi hii bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure Bonyeza Hapa kudownload App yetu bure kumbuka kuidownload kama Apk maana bado haijawekwa playstore

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post