Yanga hawapoi wamtangaza kocha Mpya Msaidizi huyu hapa
Download App ya Nijuze Tv kutazama mechi za ligi kuu Nbc bure, Epl, Laliga, Bundesliga, Seria A, Caf na nyinginezo pia app hii ina chanel za Azam tv na Dstv utaweza kuzitazama bure
Idownload kwa kubonyeza HAPA au HAPA sisi kwetu michezo ni Furaha
Yanga inaendelea na zoezi la utambulisho wa benchi la ufundi lililofanyiwa maboresho baada ya ujio wa Kocha Mkuu Romain Folz
Mabingwa hao wa Tanzania Bara kwa misimu minne mfululizo wamemtangaza Manu Rodriguez raia wa Hispania kuwa Kocha Msaidizi
Rodriguez amefanya kazi katika mataifa mbalimbali barani Ulaya na Afrika ambapo alikutana na Folz kwa mara ya kwanza mwaka 2021 wakiinoa klabu ya Ashanti Gold ya Ghana
Amejiunga na Yanga akitokea Costa Rica ambako alikuwa kocha Mkuu akihusika na timu zote kuanzia ngazi za vijana kuanzi U17, U20 na U23
Kama ilivyo kwa Folz, mwaka 2022 hadi 2024 Rodriguez alifanya kazi na FIFA akiwa mtaalam wa maendeleo katika kukuza vipaji
Anaungana tena na Folz katika klabu ya Yanga kuendeleza rekodi ya kushinda mataji, wawili hao wakipewa jukumu la kuhakikisha Yanga inafanya vizuri katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao
Usikose kuitazama mechi za michuano ya CHAN na LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA kudownload app

Post a Comment