Simba yawapiga chini Mbet yajiunga na Betway

 Simba yawapiga chini Mbet yajiunga na Betway

Download App ya Nijuze Tv kutazama mechi za ligi kuu Nbc bure, Epl, Laliga, Bundesliga, Seria A, Caf na nyinginezo pia app hii ina chanel za Azam tv na Dstv utaweza kuzitazama bure

Idownload kwa kubonyeza HAPA au HAPA sisi kwetu michezo ni Furaha

Klabu ya Simba leo imeingia makubaliano ya udhamini na kampuni ya BETWAY kutoka Uingereza. Mkataba huo wa miaka mitatu una thamani ya Tsh Bilioni 20

Akizungumza katika tukio la kusainiwa mkataba huo liliyofanyika Johari Rotana Hotel jijini Dar es salaam mapema leo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Simba Zubeda Sakuru amesema makubaliano hayo yanakwenda kuleta Mapinduzi kwenye mchezo wa mpira wa miguu hapa Tanzania

"Mkataba ambao tumeingia unakwenda kuleta mapinduzi kwenye mchezo wa soka hapa Tanzania na unakwenda kuongezea nguvu dhamira ya Simba kuwa klabu namba moja barani Afrika"

"Udhamini huu ambao thamani yake ni Bilioni 20 kwa miaka mitatu, unaonyesha namna Simba imedhamiria kuleta mabadiliko ya kuwa klabu kubwa," alisema Sakuru

Nae Mkuu wa Udhamini wa BetWay Afrika, Jason Shield amesema wameichagua Simba kufanya nayo kazi kwa sababu ni timu kubwa barani Afrika, timu inayofahamika katika pande zote la bara hili

"Tumeingia Simba sababu ni timu kubwa Afrika, ni timu ambayo inajulikana pande zote za bara hili na hilo ndio tunaangalia zaidi kwenye biashara. Tulikuwa tukiifatilia kwa miaka karibu sita lakini sasa imekuwa kweli. Tunafuraha kufanikisha jambo hili."

"Huu ni zaidi ya ushirikiano na inatakiwa klabu zote zifaidike na jambo hili. Tunashirikiana na timu nyingi kubwa ambazo tunadhamini hivyo uzoefu huo utatusaidia kufanikisha jambo hili."

"Nina furaha kwa ushirikiano huu lakini tutafanya kazi kuangalia namna gani ya kufanikisha ushirikiano na vilabu vingine vikubwa ambavyo tunashirikiana navyo," alisema

Usikose kuitazama mechi za michuano ya CHAN na LIGI KUU TANZANIA BARA, MECHI ZA ULAYA LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA kudownload app

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post