Jana Yanga ilitambulisha usajili wa kwanza katika dirisha hili, kiungo mkabaji Moussa Balla Conte aliyetua kutoka klabu ya CS Sfaxien
Conte alitua nchini mapema jana na kusaini mkataba wa miaka mtatu ambao utamuweka Jangwani hadi Julai 2028
Awali Yanga ilipanga kuanza kutoa taarifa za usajili siku ya Jumapili, Julai 20 lakini sintofahamu iliyogubika usajili wa nyota huyo ilipelekea viongozi wa Yanga kuamu kumaliza utata mapemaa kwani kuna propaganda zilikuwa zikifanywa kudai nyota huyo amegoma kucheza Yanga licha ya mabingwa hao wa nchi kumalizana na klabu yake
Huo ni usajili wa kwanza kutambulishwa, taarifa za usajili zitafahamika zaidi wiki ijayo ikiwa ni wiki ya mwisho kabla ya taratibu za pre-season kuanza
Juzi wakati akizungumza na chombo kimoja cha habari, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alidokeza kuwa mpaka sasa bado usajili wa mchezaji mmoja tu ili Yanga kufunga hesabu zake za usajili katika dirisha hili
Kwa mujibu wa taarifa za ndani, hawa hapa wachezaji ambao tayari wamemalizana na Yanga;
Mohamed Doumbia (CM)
Moussa Balla Conte (DM)
Abdulnasir Mohammed (DM)
Aboubakar Nidhar Otham (CB)
Offen Chikola (AM)
Celestin Ecua (AM)
Kwa mujibu wa taarifa, hizi hapa sajiri zinazosubiri kukamilika;
Mohammed Hussein (LB)
Feisal Salum (AM)
Aidha inaelezwa kuwa Yanga inaweza kusajili nyota wengine wawili katika nafasi ya beki wa kati na mshambuliaji hasa endapo dili la Clement Mzize kuelekea Zamalek kama litakamilika
Yanga inahusishwa na walinzi wawili raia wa DR Congo, Hennock Inonga ambaye ni mchezaji huru baada ya kumalizana na FAR Rabat na Kevin Mondeko aliyesitisha mkataba wake na USM Alger
Usikose kuitazama michuano hii LIVE bure kupitia simu yako download App hii mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi pia App bado hatujaiweka playstore hivo italeta neno This file might be harmful usiogope
Au hapa chini
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
AU BONYEZA HAPA PIA KUDOWNLOAD
Au hapa chini pia


Post a Comment