Nilizaliwa katika familia ya watoto saba kule Mbeya, nikiwa wa pili kuzaliwa. Tangu nikiwa mdogo, kulikuwa na mazoea ya kuniangalia kama mtu mwenye mikosi. Nilipoanguka darasani mara moja tu darasa la saba, mamangu alinitazama na kusema, “Wewe si mtu wa kufanikisha chochote.” Nilichukulia kama maneno ya hasira, lakini haikuishia hapo.
Nilipopata mimba nikiwa kidato cha tatu, haikuwa rahisi. Baba alichukua uamuzi wa kunifukuza nyumbani, akidai kwamba nimeiaibisha familia. Mama alilia sana lakini naye hakuwa na uwezo wa kunizuia. Nilihamia kwa shangazi yangu kule Mwanjelwa ambako maisha hayakuwa rahisi. Wakati huo ndipo niliamini kweli pengine mimi ni mkosi.
Maisha yalinizidi. Nilijaribu biashara ndogondogo ya kuuza maandazi na viazi lakini haikufua dafu. Nilipojaribu kuwaomba msaada kaka na dada zangu, walinicheka. Mmoja wao aliniambia kwa simu, “Wewe huna bahati kabisa, kila kitu unagusa kinaharibika.” Soma zaidi hapa

Post a Comment