Nisingeamini kama mtu anaweza kuja kuvuruga ndoa ya miaka 12 kwa kuhubiri ‘Mungu ameniambia nitakuwa mke wako’. Lakini ndivyo ilivyotokea. Mie ni mke wa ndoa ya kwanza, tulibarikiwa na watoto watatu, maisha yetu yalikuwa ya kawaida ila ya amani. Mume wangu alikuwa mcha Mungu, lakini alivyoanza kuhudhuria maombi kwenye kanisa jipya, alianza kubadilika taratibu.
Pale ndipo alikutana na huyu mwanamke aitwaye Rehema. Msichana wa kanisani, aliyekuwa akiombewa kila wiki kuhusu kufunguliwa ndoa. Polepole, Rehema akaanza kumtembelea mume wangu kazini, kisha kwa hila na maombi, akaingia moyoni mwake.
Nilipojaribu kuzungumza naye kuhusu hili, mume wangu aliniambia nisiingilie mipango ya kiroho. Hatimaye, akaamua kumuoa kama mke wa pili bila hata kunishirikisha.
Maisha yangu yakageuka simanzi. Rehema alianza kujivunia kwamba yeye ndiye sasa mke anayeaminika, anayeweza kumuombea mume wangu afanikiwe.
Alihama kwenye chumba kimoja cha kupanga na kuingia nyumbani kwetu, alipochukuliwa kama malkia mpya. Akaniambia mbele ya watoto wangu kwamba siku zangu zimekwisha, na sasa yeye ndiye mama wa nyumba. Soma zaidi hapa

Post a Comment