Download App ya Nijuze Tv kutazama mechi za ligi kuu Nbc bure, Epl, Laliga, Bundesliga, Seria A, Caf na nyinginezo pia app hii ina chanel za Azam tv na Dstv utaweza kuzitazama bure
Idownload kwa kubonyeza HAPA au HAPA sisi kwetu michezo ni Furaha
Msemaji wa klabu ya Singida Black Stars Hassan Masanza amesema kuwa klabu ya Simba haijalipa pesa yoyote ile kumnunua mshambuliaji wao Jonathan Sowah, wamewapa bure
Masanza ametamba kuwa hakuna klabu iliyokuwa na uwezo wa kumnunua mshambuliaji huyo kwani thamani yake ni zaidi ya Tsh Bilioni 2
"Mimi ni msemaji wa taasisi kubwa hivyo siwezi kusema jambo ambalo halipo, kilichotokea ni kuwa Simba walionesha nia ya kumhitaji Sowah na kutokana na mahusiano mazuri kati ya mlezi wetu Mheshimiwa Dk Mwigulu Nchema na Rais wa heshima wa Simba tuliwaruhusu waongee na mchezaji maslahi yake kisha tukawapa bure bila kulipa chochote" amesema Masanza.
"Unajua mlezi wetu ni kiongozi mkubwa serikalini hiyo ameamua kutoa mchango wake kwa Simba kama ambavyo amekuwa akifanya kwa vilabu vingine," alisema Masanza
Taarifa iliyotolewa Singing Black Stars mapema leo, ilibainisha kuwa Sowah amejiunga na Simba kwa makubaliano maalum
Yanga ilihusishwa na Sowah kwa muda mrefu na hata mchezaji mwenyewe aliwahi kuweka wazi kiu yake ya kuitumikia Yanga akimtaja Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ni kama baba yake hapa Tanzania
Hata hivyo Yanga iliachana na mpango wa kumsajili Sowah sababu ikielezwa ni historia yake ya matukio ya utovu wa nidhamu ambayo yamekuwa yakizigharimu timu anazozitumikia
Sowah alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa fainali kombe la CRDB dhidi ya Yanga akipewa kadi ya pili ya njano pale alipopingana na mwamuzi Ahmed Arajiga
Wadau wa soka wanasubiri kuona kama zile kauli zinazodai Singida BS ni tawi la Yanga zitaendelea au la...
Usikose kuzitazama mechi hizi leo ARSENAL vs NEW CASTLE, TANZANIA vs SENEGAL na BARCELONA vs VISSEL KOBE LIVE bure kupitia Simu yako download App yetu itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi live bure pia ndani ya App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure bonyeza HAPA kudownload app
.jpeg)
Post a Comment