Alikuwa Akinipiga Blue Tick, Sasa Ananiandika Essay za Mapenzi Kwa Paragraph

Siwezi kusahau jinsi ilivyokuwa kuingia kwenye inbox ya mtu kila siku, ukijua ataiona lakini hatarudisha. Siku moja nilimtumia “Hi 😊”   aliisoma saa ileile, lakini hakujibu. Siku iliyofuata nikatuma tena “Upo?” blue tick.



Nikamshangilia birthday yake WhatsApp, akani-reply wiki mbili baadaye na emoji ya keki tu. Blue tick ikawa kama tabia, kama marafiki wa karibu wa moyo wangu ulioumia kimya kimya.

Yote haya yalikuwa kwa sababu nilimpenda sana. Alikuwa mvuto wa jicho, mchangamfu mtaani na kila mtu alimjua. Tulikuwa tukiongea mara chache lakini mara zote nilihisi kama kuna connection fulani. Hata hivyo, mimi niliamua kupenda zaidi bila kujua kama upande wa pili ulikuwa na moyo kama wangu.



Niliona status zake kila siku memes, mazoezi, selfie. Lakini DM zangu hazikuwa zikigusiwa kabisa. Marafiki waliniambia niachane naye, wengine walinicheka: “Acha kujiabisha kwa mtu ambaye hakujui hata vizuri.” Lakini moyo wa mapenzi haueleweki ulikuwa unanivuta kwake kila siku.

Ilibidi nijikubali kuwa nimepigwa ‘blue tick ya moyo’. Nilijaribu kusahau, nilijaribu kuanzisha mazungumzo na watu wapya, lakini hakuna aliyeingia moyoni kama yeye. Soma zaidi hapa 

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post