Alicho kisema kocha mkuu wa Yanga kuelekea msimu mpya


 Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz amesema anajivunia kujiunga na klabu kubwa kama Yanga, klabu yenye historia ya kipekee barani Afrika

Folz amesema Yanga ni klabu kubwa barani Afrika ikiwa na sapoti kubwa ya mashabiki, mvuto wake umemfanya asifikirie mara mbili kujiunga na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara kwa misimu minne mfululizo

"Nafurahi sana kuwa hapa, ikiwa nitalazimika kueleza kwa nini nimechagua kuwa hapa, ni kutokana na hadhi ya klabu, historia ya klabu bila ya kusahau sapoti kubwa ya mashabiki"

"Mvuto na hamasa ya klabu ya Yanga naamini ni vitu tosha vinavyoweza kumshawishi kocha yeyote kuwa hapa," alisema Folz

Folz amesema anafahamu kazi iliyo mbele yake kwani kwa ukubwa na historia ya klabu ni lazima afanye vyema na kushinda mataji Bonyeza hapa kudownload App yenye chanel zote za Azam tv na Dstv bure yaani unaangalia bure

"Bila shaka ni lazima tupate matokeo bora zaidi, hili ni jambo la kawaida kusema kwa klabu kubwa yenye hadhi kama Yanga"

"Lakini pia tunataka kutoa burudani kwa mashabiki wetu, nitahakikisha wanapenda wanachokiona kutoka kwetu na bila shaka watakuja uwanjani kwa wingi kutuunga mkono"

"Tutahakikisha wanafurahi na kujivunia kile watakachokishuhudia kutoka kwetu uwanjani"

Folz amesema Yanga inapaswa kucheza kama timu kubwa na jukumu lake ni kuandaa mazingira ambayo yataifanya timu ifikie matarajio yake

"Mimi napenda kucheza soka la kuvutia, nataka tutawale mchezo pale tunapokuwa na mpira na hata bila mpira, tutajaribu kuwalazimisha wapinzani wetu kufanya kile tunachotaka"

"Naamini tutakuwa na mchanganyiko bora zaidi kwani falsafa yangu inalingana na matarajio yaliyopo hapa"

Usikose kuitazama mechi ya YANGA VS SAFARI LAGER CUP LIVE bure kupitia simu yako download App yetu kutazama mechi hii bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel za Azam tv na Dstv bure Bonyeza Hapa kudownload App yetu bure kumbuka kuidownload kama Apk maana bado haijawekwa playstore

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post