Klabu ya Yanga imeanza harakati za kuboresha kikosi chake kuelekea msimu ujao, kwa kulenga maeneo muhimu yenye uhitaji mkubwa wa maboresho. Moja ya maeneo hayo ni nafasi ya kiungo mkabaji, ambapo kwa sasa klabu hiyo inamtegemea zaidi Mganda Khalid Aucho.
Kiungo huyo kutoka Uganda amekuwa mhimili wa safu ya kati ya Yanga kwa misimu kadhaa sasa, lakini umri na changamoto ya majeraha ya mara kwa mara, imeibua haja ya kutafuta mbadala wa kudumu.
Katika kutekeleza mkakati huo, Yanga imevutiwa na kiungo wa Singida Black Stars, Mohammed Damaro Camara (22), ambaye alibadili uraia kuwa Mtanzania miezi michache iliyopita
Damaro amekuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Singida BS, akicheza kwa maelewano makubwa na kiungo mwingine mahiri, Josephat Arthur Bada ambaye naye ameripotiwa kuwemo kwenye rada za mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Uwezo wa Damaro katika kukaba, kupora mipira, na kusambaza pasi sahihi umeifanya Yanga kuona nafasi kubwa ya kumwingiza kikosini kama mrithi wa muda mrefu wa Aucho.
Katika kufanikisha usajili wa Damaro, Yanga inaelezwa kuwa tayari kumtoa kwa mkopo winga wa DR Congo, Jonathan Ikangalombo, kama sehemu ya makubaliano ya usajili huo.
Ikangalombo aliyetua Jangwani katika dirisha dogo la usajili, ameshindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa, na sasa anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaoweza kutolewa kwa mkopo ili apate nafasi ya kucheza mara kwa mara.
Iwapo dili hilo litakamilika, Damaro Camara ataongeza ushindani mkubwa kwenye safu ya kiungo ya Yanga ambayo pia ina wachezaji wengine kama Mudathir Yahya, Duke Abuya, Salum Abubakar na Aucho (kama ataongeza mkataba)
Usikose kuitazama mechi hii ya AFRIKA KUSINI vs TANZANIA LIVE bure kupitia simu yako download App hii mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi pia App bado hatujaiweka playstore hivo italeta neno This file might be harmful usiogope
Au hapa chini
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
AU BONYEZA HAPA PIA KUDOWNLOAD
Au hapa chini pia
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee ( ikileta neno its harmful usiogope ni kwasababu haijawekwa playstore)
- Wezesha “Unknown Sources” kwenye setting ya Simu yako. Nenda kwenye “Settings” > “Security” au “Privacy“.
Post a Comment