Klabu ya Yanga SC ya Tanzania inaendelea kufanya maboresho makubwa ya kikosi chake kuelekea msimu ujao, na sasa inadaiwa kuwa imekamilisha mipango ya kumsajili winga wa kimataifa wa Angola, Deivi Miguel Vieira 'Gilberto', anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Petro Atletico akitokea Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Hatua hii inakuja kufuatia kuondoka kwa kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki, aliyejiunga na klabu ya Wydad Athletic ya Morocco kwa dau linaloripotiwa kuwa la kuvunja rekodi.
Gilberto, ambaye kwa sasa anang'ara tena Petro Atletico, alijiunga na Pirates msimu uliopita kutoka kwa miamba hao wa Angola. Hata hivyo, alidumu kwa miezi mitano tu kabla ya kurejea kwa mkopo Januari mwaka huu, baada ya kushindwa kuzoea mazingira ya soka la Afrika Kusini.
Mashabiki wa soka barani Afrika walimshuhudia Gilberto akiangaza kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2024 nchini Ivory Coast, ambapo alifunga bao moja na kusaidia Angola kufika robo fainali ya mashindano hayo.
Katika kipindi chake Petro Atletico kabla ya kuhamia Pirates, Gilberto alionyesha kiwango bora kwa kufunga mabao 21 na kutoa assist 10 katika mechi 68 za mashindano mbalimbali, akijijengea sifa kama mmoja wa mawinga hatari zaidi ukanda wa Afrika ya Kati.
Licha ya usajili wa Jonathan Ikangalombo, benchi la ufundi la Yanga linaamini bado kuna nafasi ya kuongeza nguvu katika eneo la winga, na Gilberto anaonekana kuwa mchezaji anayefaa kuziba pengo hilo kwa ubora wake, uzoefu wa kimataifa, na uwezo wa kuamua mechi.
Iwapo dili hilo litakamilika, Gilberto atakuwa sehemu ya mpango wa Yanga kuendelea kushindana vikali katika mashindano ya ndani na ya kimataifa, hususan Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
Usikose kuitazama mechi hii ya SIMBA SC VS BERKANE LIVE bure kupitia simu yako download App yetu mapema inayorusha mechi zote live bure pia ukiwa na App yetu utaweza kutazama chanel zote za Azam Tv na DSTV live bure mfano Azam sport 1, Azam Two, Sinema zetu na nyingine nyingi pia App bado hatujaiweka playstore hivo italeta neno This file might be harmful usiogope
Au hapa chini
Kudownload Bonyeza hapa ili kudownload App
Au
AU BONYEZA HAPA PIA KUDOWNLOAD
Au hapa chini pia
App bado hatujaiweka playstore hivo utaidownload kama APK kisha uta Install kawaida tu na uendelee kufurahia chanel za Azam na Dstv bureee ( ikileta neno its harmful usiogope ni kwasababu haijawekwa playstore)
- Wezesha “Unknown Sources” kwenye setting ya Simu yako. Nenda kwenye “Settings” > “Security” au “Privacy“.
Post a Comment