Yanga yatangaza viingilio mechi dhidi ya Vital'o
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki na Wanachama wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi katika mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Vital'o
Kamwe amesema Yanga imepania kupeleka ujumbe barani Afrika siku ya Jumamosi kwa kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa katika mechi za hatua ya awali
Aidha Kamwe amewaahidi Wananchi siku hiyo wanakwenda kujaza kapu la mabao ili kuhakikisha wanaondoka na fedha za kutosha kutokana na goli la Mama
Kamwe ametangaza viingilio vya mchezo huo utakaoanza saa 1 usiku kuwa Mzunguuko na Machungwa ni Tsh 5,000/-, VIP C Tsh 10,000/-, VIP B Tsh 20,000/-, na VIP A ni Tsh 30,000/-
"Tiketi tayari zimeanza kuuzwa, nawaomba Wananchi tununue tiketi mapema tuache mazoea ya kununua tiketi siku za mwisho ili kuepuka changamoto zisizotarajiwa," alisema Kamwe
Kamwe amesema Jumamosi Yanga itazindua rasmi msimu wa ligi ya mabingwa 2024/25 kwa ushindi mnono mbele ya mashabiki wake
Aidha Kamwe amethibitisha msimu huu utaratibu wa mechi kupewa majina ya wachezaji hautakuwepo, baadae watatangaza utaratibu mpya ambao utatumika kuhamasisha mechi za Kimataifa
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment