Alichokisema Ahmed Ally baada ya Simba kuitungua Tabora united jana - EDUSPORTSTZ

Latest

Alichokisema Ahmed Ally baada ya Simba kuitungua Tabora united jana

 Usikose kuitazama mechi ya YANGA vs VITALO na SIMBA vs SINGIDA FG Live bure kupitia simu yako download app yetu itakayokuwezesha kuzitazama mechi hizi zote LIVE bure pia ukiwa na app yetu utaweza kutazama mechi zote za ulaya pia na chanel za Azam tv na Dstv bure kudownload app yetu bonyeza 👉🏻 HAPA

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United katika mchezo wa kwanza ligi kuu ya NBC, ni ishara ya dhamira ya Simba kuwania taji la ligi kuu

Ahmed ametamba kuwa mkakati wa Simba ni kuhakikisha wanaendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kushinda kila mechi inayokuja mbele yao

Hata hivyo Ahmed amewataka mashabiki wa Simba kuwavumilia baadhi ya wachezaji wapya ambao wameanza taratibu majukumu yao na Simba

Ahmed amebainisha kuwa ni jambo la kawaida kwa mchezaji anapotoka timu moja kwenda nyingine wakati mwingine huhitaji muda kuzoea

"Pamoja na kushinda dhidi ya Tabora United lakini ukweli ni kuwa tunahitaji kuwapa muda zaidi wachezaji wetu waendelee kutafuta ubora wao"

"Tumesajili wachezaji bora sana ambao wamefanya makubwa walikotoka Katika hao wapo walioanzia juu moja kwa moja na wengine wameanzia chini, iko hivyo duniani kote hasa mchezaji anapotoka timu ndogo kwenda kubwa au kutoka ligi ndogo kwenda kubwa au anapoenda kwenye timu yenye presha kubwa kama yetu"

"Ni jukumu letu kuwavumilia, kuwatia moyo, kusimama nao nyakati zote ili warejeshe kujiamini na kuupata ubora wao"

"Aina ya wachezaji tuliokua nao nusu yao wakiupata ubora wao basi mwaka huu utakua Msimu mzuri kwetu INSHA ALLAH," aliandika Ahmed katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

1 comment:

Edusportstz