Tumepewa heshima kubwa kuzindua ligi ya mabingwa - Kamwe
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema ni heshima kubwa kwa klabu ya Yanga kupewa nafasi ya kufanya uzinduzi wa msimu mpya wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Kamwe amesema wamepewa baraza zote na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kufanya uzinduzi huo Jumamosi kabla ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Vital'o ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa saa 1 usiku
Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kuendelea kununua tiketi ili kuhakikisha wanaujaza uwanja wa Benjamin Mkapa ili kuionyesha Afrika ukubwa wao
"Kwa sasa hakuna timu nyingine zaidi ya Yanga kwa Tanzania ambayo CAF wanaweza kuifikiria kufanya tukio hilo"
"Kwa hiyo tumepewa heshima kubwa kuizindua Ligi ya mabingwa hapa, Jumamosi ni siku yetu ya kufurahi, hili halijakuja bahati mbaya"
"Shamrashamra kubwa ambazo Wanayanga mlizionyesha kwenye kilele cha wiki ya Wananchi, watu wamependa jambo lile tulirudie katika uzinduzi wa ligi ya mabingwa"
"Kuna vitu vingi tumeviandaa na mengi mazuri yatafanyika siku hiyo la muhimu ni wewe shabiki na mwanachama kukata tiketi yako mapema na kuwahi Benjamin Mkapa," alisema Kamwe
Kamwe amebainisha shamrashamra za uzinduzi huo zitatanguliwa na burudani itakayoanza saa 8 mchana
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment