Simba kufunga usajili kibabe leo
Kiungo Awesu Awesu bado yuko na kikosi cha Simba kinachoendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tabora United utakaopigwa Jumapili, August 18 katika uwanja wa KMC
Jana baada Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya TFF kumrejesha Awesu kunako klabu ya KMC, uongozi wa Simba ulifungua mazungumzo na KMC kwa ajili ya kumaliza sintofahamu iliyojitokeza
Mwenyekiti wa KMC, Kheri Nassoro amethibitisha kuwepo kwa mazungumzo hayo na kudokeza jambo hilo litamalizika na Awesu ataruhusiwa kuitumikia Simba
Awali KMC walihitaji Tsh Milioni 200 dau ambalo Simba haikukubaliana nalo na hivyo kupelekea klabu hizo kukaa mezani kujadiliana ili kumaliza sakata hilo kwa maslahi ya mchezaji ambaye amesisitiza hayuko tayari kurejea KMC na kama itashindikana kujiunga na Simba basi atastaafu rasmi soka na atarejea kwao Zanzibar kuvua samaki
Dirisha la usajili linafungwa leo Alhamisi, saa 5:59 usiku bila shaka mwafaka utapatikana mapema
Katika hatua nyingine, leo Simba huenda ikatambulisha usajili wa mshambuliaji Lionel Ateba raia wa Cameroon liyetua Msimbazi akitokea klabu ya USM Alger ya Algeria
Ateba tayari yuko nchini ambapo imeelezwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuwatumikia wekundu hao wa Msimbazi
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
KUPATA KIFURUSHI CHA DATA VODA BOFYA + HAPA
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment