Baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mechi za Ngao ya Jamii, kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua amesema msimu huu amejipanga kuwapa furaha mashabiki na kuisaidia timu kufikia malengo yake
Akiwa ameingia katika mwaka wa pili wa mkataba wake, Pacome amerejea msimu huu akiwa ameimarika zaidi huku 'fitness' yake ikiwa juu
Mwisho wa msimu uliopita haukuwa mzuri sana kwake kwani alipata majeraha ambayo yalimfanya akose mechi nyingi ikiwa ni pamoja na mechi muhimu za robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns
Pacome amesema msimu uliopita ukiwa ni wa kwanza na hakuitumikia Yanga ipasavyo kutokana na majeraha, lakini sasa yuko imara baada ya kupona na zaidi ubora wa kikosi unampa msukumo mkubwa kujituma zaidi
"Kila mchezaji wa kikosi chetu hataki kufanya makosa anapopewa nafasi kwani wote ni bora, jambo ambalo linaongeza ushindani mkubwa zaidi"
"Sioni kama kuna jambo litatushinda msimu ujao, kwani mipango yetu sio kubeba makombe tu kama tulivyoanza na Ngao ya Jamii tuliyoikosa mwaka jana, pia kuwafurahisha mashabiki na viongozi kwa ujumla," alisema
Msimu uliopita Pacome aliifungia Yanga mabao matatu katika ligi ya mabingwa kuanzia hatua ya makundi. Keshokutwa Jumamosi, Yanga inaanza msimu mwingine wa michuano ya ligi ya mabingwa ambapo wataumana na Vital'o katika mechi ya mkondo wa kwanza hatua ya awali
No comments:
Post a Comment