Yanga yabadili gia angani, pre-season sasa ni Sauzi - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga yabadili gia angani, pre-season sasa ni Sauzi

Yabga sc

Mechi za EURO 2024 zinaendelea usikose kutazama mechi hizi live bure kwenye simu yako nenda playstore andika NIJUZE TV kisha download app hiyo kutazama mechi zote live bure pia kwenye app hiyo kuna muvi zilizo tafsiriwa pamoja na chanel za Azam tv na Dstv buree nenda kaidownload sasa

Kikosi cha Yanga, kinatarajia kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kuweka kambi nchini humo tayari kwa msimu mpya wa mashindano.

Yanga imekubali ombi la klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwenda nchini humo kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki mechi inayotarajiwa kupigwa Julai 17 mwaka huu wakati wa kipindi cha maandalizi ya msimu mpya yaani Pre Season.

Akizungumza nasi jana, Afisa habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema safari hii kambi yao haitakuwa Kigamboni kama ilivyo kawaida badala yake wanaelekea Afrika Kusini.

Amesema wanaelekea nchini humo kutokana na mialiko waliyoipata na kuitumia sehemu ya Pre Season hiyo kujiandaa na mashindano yaliyolo mbele yao kwa msimu ujao.

“Safari hii tunakuja tofauti na misimu ya nyuma, tunatarajia kuweka kambi Afrika Kusini, kwa mwaliko wa klabu mbalimbali na tunatakiwa kwenda Kenya kwenye ufunguzi wa uwanja wa Kisumu.

Tunatarajia kufanya ziara kwa mataifa yote tuliyoalikwa kwenda na ‘Pre Season‘ yetu itakuwa Afrika Kusini itakuwa ni sehemu tulivu kwa ajili ya maandalizi ya kikosi chetu,” amesema.


Kamwe amesema wanaimani itakuwa pre seasons nzuri kwa sababu watapata mechi za kirafiki zenye ushindani mkubwa kujianda na msimu wa 2024/25.

Takriban misimu mitatu Yanga hawakuwa kutoka kwenda nje kwa ajili ya Pre Season badala yake kutumia kambi ya Avic Town kuwa sehemu ya maandalizi.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz