Mechi za EURO 2024 zinaendelea usikose kutazama mechi hizi live bure kwenye simu yako nenda playstore andika NIJUZE TV kisha download app hiyo kutazama mechi zote live bure pia kwenye app hiyo kuna muvi zilizo tafsiriwa pamoja na chanel za Azam tv na Dstv buree nenda kaidownload sasa
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa msimu wa 2024/25 hawabahatishi katika suala la usajili kwa kuleta watu wenye ubora watakaowasahulisha wanasimba masimango waliyopata kwa misimu mitatu mfululizo.
Ahmed ameweka wazi mbichi na mbivu ya nani anabaki na kuondoka itajulikana kuanzia Jumatatu Juni 17, mwaka huu, kupisha wachezaji wapya ambao watakuja kuongeza nguvu ndani ya kikosi cha Simba kwa msimu ujao.
Akizungumza na Spotileo, Ahmed amesema kutokana na masimango waliyoyapata misimu mitatu yamemuibua Mwekezaji, Mohammed Dewji kurejea kwenye nafasi ya Uenyekiti wa Bodi na kusimamia masuala yote ya usajili.
Amesema wanaenda kufanya usajili mkubwa kwa kugusa kila nchi kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi kwa kuziba nafasi ya wachezaji watakaopewa ‘Thank You’ siku ya Jumatatu.
“Kuanzia Jumatatu ambayo ni sikukuu ya kuchinja mnyama, wachezaji wengi wataondoka na tunaanza kuwaondoa watu kwa kuwapa ‘Thank You’ kwa wale hatutawahitaji kwa msimu ujao, baada ya hapo tutawatangaza waliongeza mkataba na mwisho tutaweka wazi silaha zetu mpya.
Msimu uliopita tulichezewa sana na kupewa kila aina ya masimango hali iliyomtoa ugaibuni mwekezaji wetu kuja kushika kijiti cha usajili kwa kuhakikisha hatufanyi makosa na kuamua kuvunja Bank kwa ajili ya usajili wa nyota wapya,” amesema Ahmed.
Amewatuliza wanasimba na kuwataka kuwaunga mkono viongozi kwa sasa wapo sokoni kwa ajili ya kufanya usajili makini, msimu huu hawabahatishi kwa sababu ya mwekezaji huyo kutoangalia fedha na kutaka furaha ambayo anaipata pale Simba inapofanikiwa.
“Watakaondoka wamefanya kazi nzuri lakini hao wanaokuja ni wazuri zaidi naimani yale maneno kutoka kwa wapinzani wetu hayatakuwepo kwa sababu tunarejea katika ufalme wetu,” amesema meneja huyo.
Imeelezwa kuwa kuna wachezaji saba ambao wanatarajiwa kupewa ‘Thank You’, wakiwemo wazawa na wakigeni wakidaiwa Said Ntibanzokiza ambaye mkataba wake umetamatika, Luis Miquisssone, Pa Omary Jobe, Babakar Sar, Esomba Onana na Henock Inonga ambaye yuko sokoni baada ya Simba kupokea ofa.
Kuhusu Kocha Mkuu, Ahmed amesema hilo suala hilo lipo chini ya kamati maalum kufanyiwa kazi na anatarajia atakuja kocha mwenye kiwango kizuri na Simba kuwa salama na Agosti mwaka huu utakuwa ni mwezi wa furaha.
Post a Comment