Simba watua mezani kwa Kocha wa Mamelodi Sundowns - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba watua mezani kwa Kocha wa Mamelodi Sundowns

Mamelodi Sundowns, Steve Komphela

Bonyeza hapa kudownload app itakayokuwezesha kutazama chanel za azam tv na dstv buree pia ukiwa na app hii utaweza kutazama muvi zilizo tafsiriwa kwa kiswahili pamoja mechi zote live buree bofya sasa kudownload

Tetesi zinasema Klabu ya Simba imeripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na aliyewahi kuwa kocha wa Mamelodi Sundowns, Steve Komphela ambaye hivi sasa yupo jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kuchukua mikoba ya Abdelhak Benchikha kama kocha mkuu wa kudumu klabuni hapo.

Simba Sc ambayo imekuwa chini ya Mtanzania Juma Mgunda kwa muda inatafuta kocha mpya kwa ajili ya kampeni za msimu ujao.

Aidha zipo ripoti kuwa Juma Mgunda ameruhusiwa kuondoka klabuni hapo kwa ajili ya kwenda kukinoa kikosi cha Coastal Union.

Inadaiwa kocha mkuu wa Coastal Union, David Ouma hana sifa za kuiongoza Coastal kwenye michuano ya kombe la Shirikisho hivyo Mgunda amesaini mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya kampeni za michuano hiyo msimu ujao.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz