Kocha wa Simba Patrick Aussems atangazwa Singida Big Stars

Kocha wa zamani wa timu ya Simba SC na AFC Leopards Patrick Aussems ‘Uchebe’

Leo kivumbi cha mataifa ya africa kufuzu kombe la dunia kinaendelea ambapo kenya, uganda, burundi zitashuka uwanjani na nyingine nyingi usikose kuzitazama mechi hizi zote live bure kwenye simu yako bonyeza hapa kudownload app inayorusha mechi hizi live bure kabisa pia kwenye app hii kuna muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pamoja na chanel za azam tv na dstv bofya sasa kuidownload uweze kufurahia chanel mbali mbali

Singida Black Stars imethibitisha kuingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha wa zamani wa Simba Patrick Aussems.

Taarifa iliyotolewa jioni hii Juni 7, 2024 na kusainiwa na Ofisi ya Afisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Jonathan Kasano imesema Aussems atakuwa kocha mkuu wa timu hiyo kuanzia msimu ujao.

Aussems, ataanza kazi rasmi Julai Mosi ambapo sasa ataendelea na majukumu ya kukijenga kikosi hicho kwenye eneo la usajili, akishirikiana na uongozi wa klabu hiyo.

Aussems raia wa Ubelgiji ataanza kazi na klabu hiyo ikiwa na jina jipya ikitoka kubadilishwa kutoka iliyokuwa Ihefu ya Mbarali kabla ya kuhamishiwa Singida na kuitwa Singida Black Stars.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijaonyesha kocha huyo atakuwa na wasaidizi gani na hatma ya aliyekuwa kocha wao msimu uliopita Mecky Maxime.


Singida inakuwa klabu ya pili kwa Tanzania kumpa ajira Aussems ambaye kabla ya hapo aliifundisha Simba kwa mafanikio ikibeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara mbili na kufikisha hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post