Saido anukia Rayon Sports, Mbombo anga za KMC - EDUSPORTSTZ

Latest

Saido anukia Rayon Sports, Mbombo anga za KMC

Kiungo wa Simba SC, Saido Ntibazonkiza

Leo kivumbi cha mataifa ya africa kufuzu kombe la dunia kinaendelea ambapo kenya, uganda, burundi zitashuka uwanjani na nyingine nyingi usikose kuzitazama mechi hizi zote live bure kwenye simu yako bonyeza hapa kudownload app inayorusha mechi hizi live bure kabisa pia kwenye app hii kuna muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pamoja na chanel za azam tv na dstv bofya sasa kuidownload uweze kufurahia chanel mbali mbali

Rayon Sports ya Rwanda imetajwa kuwa kati ya timu ambazo zinapigana vikumbo kuiwania saini ya Saido Ntibazonkiza ambaye Simba imeonyesha kuwa haina mpango wa kumuongeza mkataba mpya wa kuendelea kusalia Msimbazi na tayari inaelezwa ameaga kwa wachezaji wa timu hiyo.

Rayon inataka kuboresha kikosi chake kwa ajili ya michuano ya kimataifa msimu ujao, huku pia akihusishwa na Coastal Union iliyokata tiketi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kumaliza katika nafasi ya nne katika Ligi Kuu Bara msimu uliomalizika hivi karibuni.

Nyota huyo wa kimataifa wa Burundi aliwahi kukipiga barani Ulaya kabla ya kuzichezea Yanga na Geita Gold na kunyakuliwa na Simba misimu miwili iliyopita na kutwaa tuzo ya Mfungaji Bora msimu uliopita akifunga mabao 17 akilingana na Fiston Mayele na msimu huu amemaliza mabao 11 na asisti tatu akiwa kinara wa mabao kwa upande wa Simba.

KLABU ya KenGold iliyopanda Ligi Kuu Bara msimu huu, imeanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Namungo, James Mwashinga kwa ajili ya kuongeza nguvu.

Mabosi wa KenGold wanaamini watampata nyota huyo ambaye alitua Namungo Agosti 4, 2022 akitokea Biashara United. Daudi Elibahati


UONGOZI wa KMC umeanza mazungumzo ya kumpata winga mshambuliaji wa Tabora United Mcongomani, Mbombo Jackson Impiri baada ya kuvutiwa na uwezo wake.

Nyota huyo aliejiunga na Tabora msimu uliopita baada ya kuachana na klabu ya AS Maniema Union ya kwao Congo.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz