Kibwana, Mshery wanasepa Yanga? - EDUSPORTSTZ

Latest

Kibwana, Mshery wanasepa Yanga?

Kibwana, Mshery wanasepa Yanga?

Mechi za EURO 2024 zinaendelea leo pia mechi za kirafiki nyingi zinapigwa leo usikose kuzitazama mechi zote live bure kwenye simu yako download app yetu kutazama mechi zote bure pia ukiwa na app yetu utaweza kutazama muvi zilizotafsiriwa kwa kiswahili pia utaweza kutazama chanel za Azam TV bure kudownload app yetu bonyeza 👉🏻HAPA kama utashindwa kudownload app jiunge na group letu la telegram upewe app kujiunga bonyeza HAPA

Kibwana, Mshery wanasepa Yanga?

Golikipa wa Yanga Abdutwalib Mshery na beki wa kulia Kibwana Shomari wamemaliza mikataba yao na wapo huru kujiunga na timu yoyote kama mazungumzo na uongozi wa Yanga Sc hayatakamilika.

Msimamizi wa wachezaji hao, George Job amesema wachezaji hao wameshamaliza mikataba yao na bado wanaangalia ofa kutoka timu nyingine mbalimbali zilizoomba huduma yao ingawa mazungumzo na Yanga ambayo imeonesha nia ya kuwabakiza ,bado yanaendelea.

“Kwa sasa wachezaji hao Kibwana na Msheri, wapo huru na wamepata ofa kutoka timu nyingi za ndani lakini Yanga wameonyesha nia ya kuwabakiza wachezaji hao na leo (jana) tulikuwa katika mazungumzo nao ingawa bado hayajakamilika,” ameeleza George Job.

Alisema mazungumzo hayo yalishindwa kufanyika mapema kwa sababu Yanga ilikuwa katika masuala ya kufungiwa kusajili wachezaji wa ndani na nje kutokana na madai ambayo hadi sasa wameshamalizana nayo na wapo huru kusajili ndiyo maana mazungumzo yameanza sasa.


George amesema Msheri kwa sasa yupo mapumzikoni kwa kuwa baada ya wachezaji kupewa mapumziko yeye alikuwa na timu ya taifa kule Zambia lakini pia aliporudi aliendelea kucheza katika mabonanza mbalimbali ya mechi za hisani yaliyoandaliwa na wachezaji wenzake hivyo hakupata muda mzuri wa kupumzika kama wenzake.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz