Eng. Hersi: Tutafanya kufuru usajili msimu huu - EDUSPORTSTZ

Latest

Eng. Hersi: Tutafanya kufuru usajili msimu huu

Eng. Hersi Said

Mechi za kuwania kufuzu kombe la dunia kwa mataifa ya africa na nje zinaendelea leo usikose kuzitazama mechi hizi live bure kwenye simu yako bonyeza hapa kudownload app inayoonesha mechi hizi live buree kabisa kwenye simu yako pia ukiwa na app hii utaweza kutazama muvi zilizo tafsiriwa kwa kiswahili pamoja na chanel zote za azam tv na Dstv bure bofya sasa kuidownload

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema umepanga kusajili wachezaji wachache kuelekeea msimu ujao, lakini wenye uwezo mkubwa kama waliopo au zaidi yao.

Rais wa Klabu hiyo, Injinia Hersi, amesema pamoja kuwa na kikosi kizuri, bora na imara, bado wataongeza baadhi ya wachezaji wachache, lakini wenye viwango vya hali ya juu kama waliopo  au zaidi kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi kuelekea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao. 

Alisema kama kawaida yao, wapo makini katika suala ya usajili, hivyo kuwataka wanachama na mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi. 

"Tumedhamiria kuwa na kikosi bora zaidi kitakachotikisa Afrika, kwa hiyo tutafanya usajili wa wachezaji watakaokuwa na faida ndani ya timu na kikubwa tunawekeza kwenye michuano ya Afrika, ili tufanye vyema huko tunalazimika kufanya usajili utakaoongeza nguvu ya kututoa hapa tulipo na kufikia kule tunapotarajia, tunataka kuwa na akina Pacome au Aziz Ki wengi ndani ya kikosi" alisema Hersi. 

Mbali na hayo alisema kwa sasa wanaendelea kuwaongeza mikataba wachezaji ambao wanaona wanafaa kuendelea nao kwa matakwa ya benchi la ufundi, huku wale ambao wataonekana hawakidhi mahitaji ya klabu watawapisha wapya kuendelea pale walipoishia. 

Alisema lengo la uongozi ni kuona timu hiyo inafanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo tayari wameshakata tiketi ya kushiriki baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara. 

"Msimu hyuu tumeishia robo fainali japo malengo yetu yalikuwa hatua ya makundi, msimu ujao tunataka kufika mbali zaidi, na kuw amiongoni mwa timu kubwa na tishio Afrika, hii ndio sababu tunafanya usajili wa maana na wenye tija," alisema Hersi.  

Yanga pamoja na kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara mara ya tatu msimu huu, lakini imekuwa na kiwango bora na msimu wenye mafanikio, ambapo mbali na ubingwa huo, imetwaa Kombe la FA, pamoja na kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikitolewa kwa mbinde na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwenye hatua hiyo. 

BONYEZA HAPA KUTAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz