Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeahirisha rasmi michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 na badala yake itafanyika Januari 2026.
Uamuzi huu umefanywa ili kuepusha mgongano wa ratiba na Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA, linalotarajiwa kuanza Juni 15 hadi Julai 13, 2025, nchini Marekani.
Tarehe za awali za AFCON zilikuwa Juni 2025, hivyo Kupangwa upya huku kunamaanisha kuwa AFCON na Kombe la Dunia la FIFA 2026 zitafanyika mwaka huo huo, tofauti ikiwa ni miezi sita pekee.
Una maoni gani juu ya uamuzi huu?
Post a Comment