Hatma ya Kiungo Mshambuliaji wa Simba anayelipwa mshahara mkubwa zaidi klabuni hapo, Luis Miquissone ipo mikononi mwa Uongoozi wa timu hiyo.
Wakati huu wa usajili wa dirisha kubwa, ambalo pia uhusisha na taarifa za baadhi ya wachezaji kutemwa kwenye timu zao, kwa kuvunjiwa mikataba au kuuzwa na kuachwa huru, kesi hii huenda ikamkuta nyota huyo ambaye kwa msimu uliomalizika hakuwa na kiwango kizuri.
Simba inaendelea kujipanga zaidi, huku ikiangali namna ya kuachana na nyota wake ambao hawakuwa na wakati mzuri uwanjani, licha ya kupatiwa nfasi ya kuonesha uwezo.
Moja kati ya wachezaji ambao ameleta mgawanyiko na makundi sio tu kwa mashabiki bali hata kwenye Uongozi, juu ya hatma yake ni Luis Miquissone aachwe au aendelee kwa msimu uliobakia, lakini je akivunjiwa mkataba gharama zake zikoje? endelea kusalia nasi…
Luis Miquissone wakati anarejea Simba alisaini mkataba wa miaka miwili,hivyo hadi sasa amebakiza mwaka mmoja,rasmi atakuwa huru june 30/2025.
Miquissone ni mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa kuliko wote Simba na ni miongoni mwa wachezaji wawili wanaolipwa hela nyingi ligi kuu bara. Kiasi cha Tsh milioni 47.
Pia kwenye mkataba wake kuna bonasi mbalimbali mfano akifunga goli anapewa $200 na akitoa pasi ya goli anapewa $100 ila kwa bahati mbaya hakuwa na msimu mzuri.
Kubwa zaidi kwenye mkataba wa Luis Miquissone na Simba kuna kipengele cha kuvunja mkataba huo mwishoni mwa simu huu endapo Simba hawatoridhishwa na kiwango chake.
Na mkataba huo ukivunjwa Simba hawatatakiwa kumlipa chochote. Hivyo hatima ya Luis Miquissone iko mikononi mwa viongozi wa Simba.
Kwenye jambo hili viongozi wa Simba wanastahili sifa na pongezi walicheza kama Chama anapokuwa ndani ya boksi la mpinzani huwa anatulia, Kipengele hiki kinawaweka Simba sehemu salama endapo wataamua kumvunjia mkataba Luis hawata ingia gharama ya kumlipa fidia.
Post a Comment