Tumemkosa Aziz Ki sasa tunamtaka Gamondi - Kaizer - EDUSPORTSTZ

Latest

Tumemkosa Aziz Ki sasa tunamtaka Gamondi - Kaizer

Tumemkosa Aziz Ki sasa tunamtaka Gamondi - Kaizer

Kudadeki ni Jumamosi hii Yanga vs Simba mechi ya kibabe mechi ya Kisasi usikose kuitazama mechi hii live bureee kupitia Simu yako bado unajiuliza utaitazama vipi au wapi bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii live buree kabisa hakika ni mechi ya Kibabe bofya kudwownload mapema ili usipitwe

Klabu ya Yanga juzi ilishuka dimbani na kufanikiwa kupata pointi tatu muhimu mbele ya Singida Fountain Gate, lakini kuna jambo moja limeishtua klabu hiyo likiibukia kutoka Afrika Kusini.

Inaelezwa wakati Yanga ilipokuwa Sauzi ikicheza na Mamelodi Sundowns, klabu kubwa ya huko Kaizer Chiefs ilikuwa inapiga hesabu ikiwa jukwaani na fasta ikalichukua jina la kocha wa wababe hao wa Ligi Kuu Bara, yaani Miguel Gamondi.

Kaizer Chiefs maarufu kama Amakhosi wamelichukua jina la Gamondi katika mchujo wa mwisho baada ya kushusha sapraizi ya kuwabana Mamelodi nyumbani baada ya awali kuwabana Kwa Mkapa jambo liiliwashtua mabosi wa Kaizer wakiona kama kocha huyo Muargentina anaweza kuja kuwa suluhisho la kusitisha ufalme wa Mamelodi katika Ligi ya PSL.

Hatua ya kushtua zaidi kwa Yanga ni Gamondi mkataba wake na Yanga umebakiza miezi tu kabla ya kumalizika mwisho wa msimu huu, kitu kilichowaongezea mzuka mabosi wa Kaizer kuliweka jina lake mezani.


Kama mnakumbuka wakati Yanga inarejea kutoka Afrika Kusini, Gamondi alishtua zaidi alipozungumza kwa kusema bado hana uhakika kama ataendelea na Yanga kwa msimu ujao, kauli iliyoongeza presha kwenye mustakabali wa kocha huyo klabuni hapo.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz