Klabu ya Yanga imesema kuwa wachezaji wao wote waliokuwa kwenye majeraha wameanza kurejea polepole kwenye kikosi hicho kwa ajili ya maandalizi kueleka dabi ya Kariakoo dhidi ya watani zao Simba SC.
Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe wakati akizungumza na wanahabri kuelekea mchezo huo utakaopigwa Jumamosi, Aprili 20 katika Dimba la Mkapa.
“Tumerejea leo (jana) kutoka Mwanza, na leo (jana) ni mapumziko lakini kesho (leo) timu itaingia kambini Avic Town kuanza maandalizi rasmi kuelekea dabi. Wachezaji wetu kwa asilimia kubwa waliokuwa na majeruhi wameanza kurudi. Mmemuona Mauya, Kibwana, Aucho yupo, Yao naye amesharudi yupo tayari.
“Musonda alikuwa na injury ndogo sana, Pacome naye alikuwa kwenye hatua za mwisho za recovery tukaona tusiwalazimishe hawa wachezaji kucheza hizi mechi zilizopita tukawatia kwenye hatari zaidi. Yanga tuna kikosi hatuna timu na kila aliyesajiliwa kwenye kikosi chetu anaweza kucheza akatupa matokeo mazuri.
"Tunaomba Mungu wale wachezaji waliokuwa na majeruhi wawe wamepona, tukutane Aprili 20, tukiwa kamili, watatupa tu pointi tatu, watatupa tu. Pacome anaendelea vizuri, kesho (leo) ataingia kambini na tutakuwa nae Aprili 20.
“Kwa hiyo ishu ya Musonda sio kubwa na sasa yuko vizuri, Pacome naye ameingia kwenye hatua za mwisho. Jumamosi Yanga itakuja kamili kikubwa, kiroho mbaya na kikatiri kwa ajili ya huu mchezo. Mchezo huu tunauchukulia kama mchezo wa ubingwa na mchezo wa heshima.
“Yanga ilivyojuiandaa kucheza na Mamelodi Sundowns ni mara kumi ya vile tulivyojiandaa kucheza na Simba. Wachezaji wapo tayari asilimia 100 na lengo letu ni ushindi. Karibuni sana uwanjani," amesema Kamwe.
No comments:
Post a Comment