Mayele: Nipo tayari kutua Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Mayele: Nipo tayari kutua Simba

Mayele: Nipo tayari kutua Simba

Leo ndio kivumbi na Jasho kudadeki usikose kuitazama mechi ya Al ahly vs Simba live buree kabisa bonyeza hapa kudownload app itakayorusha mechi hii buree kabisa bofya sasa kuidownload ili usipitwe

Mshambuliaji wa Pyramids FC ya Misri, Fiston Kalala Mayele amefanya mahojiano ya Simba TV kuelekea mchezo wa robo fainali ya CAFCL kati ya Al Ahly na Simba SC utakaopigwa leo nchini humo.

Akihojiwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, Mayele ambaye amewahi kukipiga katika Klabu ya Yanga amesema kuwa Simba wanayo nafasi ya kufanya vizuri endapo watarekebisha mambo machache.

Ahmed: Wewe unaijua vizuri Ally Ahly, ubora wao na udhaifu wao upo wapi?

Mayele: Ni kweli kwa sababu tunacheza ligi moja, lakini Al Ahly ya msimu huu imeshuka kiwango tofauti na misimu iliyopita. Hawajafanya usajili sana wanatumia wachezaji walewale miaka yote, wachezaji nao wanachoka kwa sababu mechi ni nyingi na mashindano ni mengi.

Ahly wakiingia hatua kama hii (robo fainali) wanabadilika. Hapa Misri mechi kuahirishwa ni ngumu lakini wao wamepambana mpaka wameruhusiwa kusogezewa mbele mechi zao ili wajiandae vizuri kucheza na nyinyi, kwa hiyo wamejiandaa kwelikweli.

Ahmed: Simba wafanye nini kupata ushindi?

Mayele: Hapo ni kutembea mtu na mtu, kila anapokanyaga upo mpaka waseme leo kazi tunayo. Mechi kama hii inahitaji watu wenye uwezo wa kuamua mechi wenyewe, Simba wanaye Chama.


Aidha, Mayele amesema kuwa kuhusu kutua Simba, lolote linaweza kutokea msimu ujao.

Ahmed: Wanasimba wanakusubiri kwa hamu

Mayele: Tumuombe Munguvtumalize msimu salama, InshaAllah chochote kinawezekana.

JIUNGE NA GROUP LA WAKUBA HAPA 18+ HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPADownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz