Hawa hapa wachezaji wa Yanga watakao ikosa mechi ya leo dhidi ya Dodoma Jiji - EDUSPORTSTZ

Latest

Hawa hapa wachezaji wa Yanga watakao ikosa mechi ya leo dhidi ya Dodoma Jiji

Pacome, Yao, Musonda kuikosa Dodoma, Aucho yupo fiti

Ni leo Dodoma Jiji vs Yanga usikose kuitazama mechi hii Live bureee kupitia simu yako bonyeza hapa kudownload app inayirusha mechi hii bure kabisa

Meneja wa Young Africans SC, Walter Harson, amezungumzia maandalizi na hali ya kikosi kuelekea mchezo wao wa leo Jumatano dhidi ya Dodoma Jiji.

Mchezo huo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB Bank, unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kuanzia saa 2:00 usiku.

Rekodi zinaonesha kwamba, timu ya Young Africans tangu ipoteze kwa goli 1-0 Julai 25, 2021, imefanikiwa kucheza michezo 14 mfululizo ya michuano hiyo bila ya kupoteza, huku ikibeba ubingwa wake mara mbili mfululizo, msimu wa 2021-2022 na 2022-2023.

Harson amesema: “Pacome Zouzoua, Yao Kouassi Attohoula bado wanaendelea na ‘recovery’ tunategemea kwenye mchezo ujao wanaweza wakawa sehemu kama kila kitu kitaenda sawa.

“Kennedy Musonda alipata ‘knock’ katika mchezo uliopita dhidi ya Mamelodi na hayuko sehemu ya kikosi kwa siku ya leo (jana), anaendelea na physiotherapy na tunategemea mchezo ujaoj anaweza kuwepo.

“Watu hao watatu ndio hawapo na hawatakuwa sehemu ya mchezo, lakini wengine wote wapo tayari kuweza kuwawakilisha Wananchi katika siku ya kesho (leo

Itakumbukwa kuwa, kiungo mkabaji raia wa Uganda, Khalid Aucho alifanyiwa upasuaji mdogo wa goti na kumsababisha kukaa nje kwa wiki kashaa baada ya kuumia kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly, lakini sasa yupo fiti kuingia uwanjani na kupambania timu yake.


NENO KWA WANANCHI

“Mashabiki wa Wananchi kama ambavyo imekuwa kawaida yenu, mmekuwa mkitupa sapoti kubwa sana ndani na nje ya nchi, sasa tupo Dodoma. Mashabiki wa Dodoma na walio karibu kwa maana ya Iringa, Morogoro, Arusha, kesho ni siku nyingine ambayo tuna nafasi ya kuhakikisha tunakuwa sehemu ya mafanikio ya Young Africans.

“Karibuni sana kwenye Uwanja wa Jamhuri mje kutupa sapoti na tunaamini kabisa tunaenda kwenye hatua ya robo fainali kwa sapoti ambayo itatoka kwenu, karibuni mtupe sapoti na sisi tunaahidi hatutawaangusha.”



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz