Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, asema kutokana na matokeo wanayoyapata, wanapaswa kujitathimini kabla ya msimu kuisha.
Akizungumza jana mara baada ya kufurushwa kwenye mashindano ya CRDB Confederation Cup na Mashujaa FC, Ahmed alisema, anawapa Pole mashabiki wote wa Simba na kikubwa kwa sasa ni kila mmoja kujitathimini.
"Sisi viongozi tunapaswa kujitathimini, benchi la ufundi, wachezaji kila mmoja anapaswa kujitathimini kuona je tunakosea wapi na nini tufanye kurekebisha kabla ya kufanya tathimini ya jumla mwisho wa msimu," alisema Ahmed.
Ahmed alisema, kama taasisi ilikuwa na malengo ya kuchukua vikombe ambavyo vingi tayari wamevipoteza na wamebakiwa na Ligi Kuu pekee hivyo wanapaswa kufanya mabadiliko makubwa mwishoni mwa msimu.
No comments:
Post a Comment