Chama atoa kauli ya kibabe kuhusu mechi yao na Al ahly - EDUSPORTSTZ

Latest

Chama atoa kauli ya kibabe kuhusu mechi yao na Al ahly

Chama: Na Ahly ni ngumu, lakini msihofu

Kudadeki unaanzaje kukosa mechi ya Al ahly vs Simba bonyeza hapa kudownload app itakayo kuwezesha kuitazama mechi hii Live bureee kabisa bofya sasa kuipakua mapema kabisa ili kuepuka usumbufu siku ya mechi

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amesema wanakwenda kushambulia ili kupata matokeo dakika za mapema licha ya mlima mrefu walionao katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji Al Ahly utakaopigwa keshokutwa, Ijumaa huko Cairo, Misri.

Simba itashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza kwenye uwanja wake wa nyumbani baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0.

Akizungumza na Mwanaspoti, Chama amesema hawatarajii mteremko, bali wanategemea ugumu dakika zote 90 na wanajiandaa kwenda kushindana bila kujali matokeo yaliyopita, huku akiweka wazi kuwa hawaendi kujilinda, bali watafunguka ili wapate matokeo dakika za mapema.

"Kupoteza kwenye uwanja wetu wa nyumbani ni sehemu ya matokeo na haitufanyi tukubali kushindwa. Bado tuna dakika 90 ngumu ugenini kama wenzetu waliweza kutufunga nyumbani na sisi tuna nafasi ya kuwafunga kwao," amesema.

"Tulicheza vizuri uwanja wa nyumbani hatukuwa na bahati tunakwenda Misri kushambulia na kuhakikisha tunapata matokeo dakika za mapema za mchezo ili kuturudisha kwenye ushindani."

Chama amesema wanawaheshimu wapinzani wao huku wakiwa na mbinu za kuhakikisha wanakuwa imara dakika za mapema ili kujitengenezea mazingira ya kufanya kitu kitakachowapa nafasi ya kusonga hatua inayofuata.


"Benchi la ufundi limeona upungufu tuliofanya na tayari limeanza kufanyia kazi kabla ya mchezo huo muhimu kwetu ambao utatupa nafasi ya kusonga hatua inayofuata endapo tutafanyia kazi yale ambayo tayari tumeanza kuelekezwa," amesema.

"Tuna kocha mwenye uzoefu ambaye ametoka kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika ukichanganya na wachezaji ambao tumepata nafasi ya kucheza hatua ya robo fainali zaidi ya misimu miwili kuna kitu kimeongezeka."

Simba ilianza mazoezi juzi na kesho inaanza safari kwenda Misri tayari kwa ajili ya kusaka kutinga hatua inayofuata.

JIUNGE NA GROUP LA WAKUBA HAPA 18+ HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz