Msemaji wa Klabu ya Azam, Hasheem Ibwe amesema kuwa licha ya kutoa sare kwenye mechi za hivi karibuni, kikosi chao kipo vizuri na bado wanayo matumaini makubwa ya kuutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC msimu huu.
Ibwe amesema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Coastal Union jana na kuambulia sare ya bao 1-1 huku akiwachimba mkwara Yanga kuelekea mchezo wao wa Machi 17 akidai kuwa watawashangaza siku hiyo kwa kuwapa kipigo kikali.
“Sisi sio wanyonge na nilisema tangu mchezo uliopita kwamba tunataka ubingwa kwa sababu inawezekana. Hakuna mtu aliyeamini kwamba jitu linaweza kupigika leo Morogoro likamwagika (kipiho cha Simba dhidi ya TZ Prisons), kwa hiyo viporo vina chacha na mechi zinakuwa ngumu.
“Azam FC kwenye ubingwa tupo, naendelea kusisitiza hilo. Na ili upambane na wanaoutaka ubingwa lazima ufue timu kama hizo ambazo zina tabia ya ubingwa ubingwa.
“Mechi ya Machi 17, ni nyepesi kwetu sisi kama timu. Tuko tayari kwa hilo. Watu wasije wakadanganyika kwa hizi sare tunazopata au kwa namna tunavyocheza kwamba hatuna mshambuliaji, sisi tunayo timu na mwalimu wa mpira haswa.
“Nina uhakika mashabiki wanajua tunaweza kufanya nini hasa kwenye mechi kubwa kama hizi,” amesema Ibwe.
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment