Kikosi cha Yanga kiko Ruangwa kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa baadae leo saa 12 jioni katika uwanja wa Majaliwa
Ni mechi muhimu kwa Yanga kwani ushindi utawashuhudia wakirejea kileleni mwa msimamo wa ligi
Hata hivyo Namungo Fc hajawahi kuwa mpinzani mwepesi kwa Yanga hivyo ni mechi ambayo itakuwa ngumu
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana jijini Dar es salaam Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Mudathir Yahya katika dakika ya 88
Wananchi leo wanatarajiwa kuwakosa badhi ya nyota wao ambao wamebaki jijini Dar es salaam kutokana na majeraha na matatizo ya kifamilia
Djigui Diarra, Khalid Aucho, Joyce Lomalisa na Pacome Zouzoua sio sehemu ya wachezaji ambao wako Ruangwa
Pengine Wananchi leo watarajie kumshuhudia Maxi Nzengeli akirejea kikosini wakati Augustine Okrah huenda akapata nafasi ya kuanza katika mchezo huo
PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE HAPA
No comments:
Post a Comment