Aucho rasmi Uwanjani, Yao ishu ipo hivi..! - EDUSPORTSTZ

Latest

Aucho rasmi Uwanjani, Yao ishu ipo hivi..!

Aucho rasmi Uwanjani, Yao ishu ipo hivi..!

Bonyeza hapa kudownload app yetu ili uweze kutazama mechi ya Yanga vs Mamelodi live ( mubashara ) bureeee kabisa hakuna kulipia ni mb zako tu unachelewa nini sasa bofya sasa

Yanga inarudi kwenye uwanja wa mazoezi leo Jumatatu kuendelea na maandalizi ya kukutana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, lakini nje ya uwanja kuna kazi inafanywa na daktari mmoja aliyewahi kushtua kumrudisha uwanjani mapema kipa Aboutwalib Mshery, ambaye sasa amejifungia na beki Yao Kouassi.

Yao ameumia nyama za paja na kwa mujibu wa taratibu za kawaida anaweza kutumia wiki mbili au tatu kupona sawasawa, lakini daktari Youssef Ammar amejivalisha mabovu akipambana kumuwahisha kabla ya hapo ikiwezekana kuwahi mechi dhidi za Mamelodi Sundowns kama sio ya nyumbani basi ya ugenini.

Youssef ambaye ndiye aliyemfanya winga Bernard Morrisson arejee chini kufuata matibabu yake, kwa sasa akili yake inapambana na Yao kwa matibabu ya vipindi vinne tofauti asubuhi, mchana, jioni na hata usiku kuangalia kama anaweza kumnusuru beki huyo wa kulia tegemeo la kikosi cha Miguel Gamondi.

Mbali na Yao, Youssef pia anafuatilia kila hatua ya maendeleo ya kiungo Pacome Zouzoua aliyepo na timu ya taifa ya Ivory Coast iliyokuwa Ufaransa huku habari njema kwa mashabiki wa timu hiyo ni kuwa jamaa alianza kuchezea mpira japo aliishia kukaa benchini wakati timu hiyo ikitoka sare ya 2-2 na Benin.

Hofu ya wanayanga ni kutokana na ukweli beki mwingine wa kulia anayepokezana na Yao, Kibwana Shomary naye ni majeruhi, japo Dickson Job anayecheza kama beki wa kati huwa anatumika kulia pale kunapokuwa na changamoto kama hiyo ya majeruhi kwa mabeki wote wa pembeni.

“Jamaa (Ammar) anapambana kuona Yao anakuwa fiti mapema, ili atumike japo tunasubiri kuona inakuwaje, ila ni mtu aliyewasaidia kupona kwa haraka hata Yacouba Songne, Mshery na amvutia Morrison aliyeamua kuja Tanzania kutoka Morocco anakoichezea FAR Rabat,” alisema mmoja wa vigogo wa Yanga.

AUCHO SASA RASMI

Wakati ishu ya Yao ikiwa hivyo, kwa sasa ni rasmi kwa mashabiki wa Yanga, kwamba kiungo Khalid Aucho amerejea uwanjani na leo ataanza mazoezi na kikosi kizima cha timu hiyo baada ya kufuzu vipimo vya uponaji wa jeraha la upasuaji mdogo wa goti aliofanyiwa hivi karibuni na kumkosesha mechi nne za Ligi.


Aucho aliyeumia katika mechi ya mwisho ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly, alikosa mechi za ligi dhidi ya Namungo, Ihefu na Geita Gold ambapo Yanga ilishinda kwa kishindo na ile ya Azam FC iliponyooshwa mabao 2-1 Kwa Mkapa.

Kiungo huyo raia wa Uganda, alikuwa na mazoezi makali ya siku tisa na Youssef ambaye ni daktari wa viungo ambapo wikiendi iliyopita alimaliza taratibu zote za vipimo na sasa anajumuishwa na wenzake ukisalia uamuzi wa kocha Miguel Gamondi kumtumia kwenye mechi ijayo.

Mbali na Aucho pia beki Ibrahim Hamad ‘Bacca’, viungo Mudathir Yahya na mshambuliaji Clement Mzize ambao walirejea nchini kutoka kambi ya timu ya Taifa Stars nao wataanza maandalizi hayo na wenzao.

Yanga itakutana na Mamelodi katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya timu hizo kurudiana Aprili 5 mjini Pretoria, Afrika Kusini na mshindi wa jumla atasonga mbele kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.

JIUNGE NA GROUP LA WAKUBA HAPA 18+ HAPA


PATA GB 30 KILA MTANDAO BURE  HAPA



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz