Yanga yaingia mkataba Tuzo za mchezaji Bora kila mwezi - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga yaingia mkataba Tuzo za mchezaji Bora kila mwezi

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
National Insurance Cooperation (NIC) imeingia mkataba na Yanga kwa ajili ya kutoa tuzo za mchezaji bora wa Yanga ambazo zitatolewa kila mwezi


Mkataba huo wa miaka mitatu una thamani ya Tsh Milioni 900


Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema mkataba huo matokeo mazuri ya uhusiano kati ya Yanga na NIC akiamini utawapa fursa wachezaji wa Yanga kutuzwa katika kila mwezi


"Mkataba huu ni wamiaka mitatu na thamani yake itakuwa milioni 900. Mkataba huu utakuwa unalenga moja kwa moja kwa mchezaji bora wa mwezi,tunakuhakikishia mkataba huu utakupa thamani sahihi ya kile ulichokiwekeza kwetu"


"Kwetu sisi kama Yanga Sc ni heshima kubwa sana kufanya kazi na kampuni kubwa kama hii kutokana na utendaji wetu sahihi ndani ya klabu yetu"


"Tunakuakikishia ushirikiano mkubwa sana toka kwetu na tunakuakikishia tutakwenda mbali zaidi ya hapo sisi na kampuni yako," alisema Hersi


Tuzo ya mchezaji bora itaanza mwezi huu Oktoba ambapo mwanzoni mwa mwezi Novemba wachezaji watatu waliofanya vizuri Oktoba watapigiwa kura na mashabiki ili kumpata mshindiDownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz