Tetesi: Chuma hiki kumrithi Konkoni Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Tetesi: Chuma hiki kumrithi Konkoni Yanga

 Benson Omalla

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Taarifa kutoka ndani ya Klabu Yanga zinaeleza kuwa, timu hiyo inahusishwa kumnyemelea mshambuliaji wa Gor Mahia, Benson Omalla Ochieng katika usajili wa dirisha dogo mwezi Januari ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.


Omalla ambaye ni raia wa Kenya amekuwa na kiwango kizuri tangia msimu uliopita na msimu huu, alikuwa chaguo la pili la Yanga baada ya Hafiz Konkoni wakati wa usajili lakini hatimae Yanga wakamsajili Hafiz Konkoni kutoka Becham ya Ghana.


Hata hivyo, Mghana huyo ameshindwa kuonesha makali yake na huenda akatolewa kwa mkopo katika dirisha dogo la mwezi Januari.


Yanga pia wanaye mshambuliaji kutoka Zambia, Kennedy Musonda aliyesajiliwa katika dirisha dogo la msimu uliopita lakini bado hajaonyesha makali kama ambavyo Yanga walitarajia na badala yake washambuliaji wote hao wamekuwa wakiwekwa benchi na mzawa, Clement Mzize.



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz