Fei Toto hana furaha Azam, anataka kutimkia Simba - EDUSPORTSTZ

Latest

Fei Toto hana furaha Azam, anataka kutimkia Simba

 Fei hana furaha Azam, anataka kusepa Simba

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga SC ambaye kwa sasa anakipiga Azam FC, Feisal Salum Abdallah 'Fei Toto' hana furaha ndani ya klabu ya Azam, hivyo anataka kusepa.


Chanzo cha karibu cha mchezaji huyo kimenithibithia kuwa Fei anataka kucheza Klabu ya Simba msimu ujao timu kongwe kubwa na bora ukanda huu wa CECAFA.


Chanzo hicho kimeeleza kuwa malengo yake ni kujitangaza Afrika nzima imjue na hawezi kufikia malengo hayo kama ataendelea kubakia kucheza Azam, timu ambayo haiwezi kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu au kumaliza nafasi ya pili ili ipate tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, CAF Champions League.


Fei Toto anasema timu pekee itakayofanya aonekane Afrika nzima na afike mbali kimataifa ni Simba SC pekee kwa sasa ndio anaiona timu yenye malengo makubwa ya kuliteka soka la Afrika.


"Fei kama kijana mdogo mwenye ndoto za kufika mbali anatamani sana kucheza Simba atafanya kila linalowezekana ili atue kwenye klabu hiyo ambayo itatimiza ndoto zake kwa vitendo na sio maneno," kimesema chanzo hicho.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz