Yanga yapania kulipa kisasi dhidi ya El merrikh - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga yapania kulipa kisasi dhidi ya El merrikh

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga wana dakika 180 za kuamua hatma yao katika hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika wakikabiliwa na mchezo dhidi ya Al Merrikh ya Sudan


Mchezo wa mkondo wa kwanza utapigwa Septemba 16 nchini Rwanda na mchezo wa marudiano kupigwa jijini Dar es salaam kati ya Septemba 28-30 katika uwanja wa Azam Complex


Ni dakika 180 za jasho na damu kwa Wananchi kuhakikisha wanamaliza ukame wa kutocheza makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa zaidi ya miaka 20


Aidha ni dakika 180 za kisasi dhidi ya Al Merrikh ambapo katika mechi zote za mtoano, Yanga haijawahi kuwatoa


Takwimu zinaonyesha timu hizo zilikutana hatua ya mtoano ligi ya mabingwa mwaka 1973, Al Merrikh wakishinda mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa Tanzania na sare ya bao 1-1 katika mchezo wa mkondo wa pili uliopigwa huko Sudan


Katika mechi sita za mashindano ambazo timu hiyo zimekutana, mechi nne zilimalizika kwa matokeo ya sare huku Al Merrikh wakishinda mechi mbili


Yanga itakuwa ikisaka ushindi wake wa kwanza dhidi ya wababe hao wa soka kutoka Sudan


Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi pamoja na kuwa Yanga itakuwa na faida zaidi kwani Al Merrikh mchezo wao wa nyumbani hawatacheza kwao Sudan


Ni kutokana na machafuko yanayoendelea huko Sudan, Al Merrikh walitumia uwanja wa Pele, Kigali katika mchezo wao wa hatua ya awali


Jitihada za kuhamishia Morocco mchezo dhidi ya Yanga ziligonga mwamba na hivyo Al Merrikh kulazimika kubakia Rwanda


Kwa mazingira yanayowakabili Al Merrikh ni wazi Yanga ina kila sababu ya kupata matokeo ya ushindi na kusonga mbele hatua ya makundi


Yanga inaendelea na maandalizi chini ya kocha Miguel Gamondi kikosi kikitarajiwa kusafiri kwenda Rwanda Alhamisi, Septemba 14Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz