Tutapeleka mabasi 100 Rwanda : Ally Kamwe - EDUSPORTSTZ

Latest

Tutapeleka mabasi 100 Rwanda : Ally Kamwe

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wanatarajia kuwa na zaidi ya mabasi 100 yatakayobeba mashabiki kuelekea Rwanda kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Merrikh


Mchezo huo utapigwa Jumamosi Septemba 16 2023, kikosi pamoja na msafara wa mashabiki ukitarajiwa kuondoka Alhamisi ya Septemba 14


"Mpaka sasa tumejaza mabasi 28, haya yanajumuisha mikoa yote, zoezi la uandikishaji bado linaendelea tukitarajia kuwa na mabasi zaidi ya 100"


"Kwa wale wa mikoa jirani na Rwanda, utaratibu unaandaliwa katika Matawi, kwa wale wa jijini Dar es salaam gharama ni Tsh 150,000/-, Wasiliana nasi kupitia namba ya simu tuliyotoa au fika Makao Makuu ya klabu kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kusafiri muhimu lazima uwe na hati ya kusafiria," alisema Kamwe


Katika hatua nyingine, kiungo wa zamani wa Yanga Haruna Niyonzima amewakaribisha Wanachama na mashabiki wa timu hiyo katika mchezo dhidi ya Al Merrikh


"Tunafuraha sana kusikia mnakuja nyumbani, tutawapokea vizuri, nawaomba Wanyarwanda wenzangu washirikiane na mimi ili kuipokea timu yetu vyema. Nawaombea muwe na mchezo mwema ili muanze mashindano haya vizuri," alisema Niyonzima


Yanga imepania kutinga makundi ya ligi ya mabingwa hivyo inahitaji kuanza vyema mchezo wa mkondo wa kwanza ugenini kumbuka mechi hii itakuwa live kweñye app yetu kama bado huna app yetu 👉👉 BOFYA HAPADownload our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz