Morrison atambulishwa rasmi FAR Rabat ya Morocco - EDUSPORTSTZ

Latest

Morrison atambulishwa rasmi FAR Rabat ya Morocco

 Morrison18874Aliyekuwa kiungo wa Klabu ya Yanga, Bernard Morisson ametangazwa radmi kuwa mchezaji mpya wa As FAR RABAT ya Morocco.

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Hivi karibuni,  iliripotiwa kuhusu kukamilika kwa dili hilo la Morrison raia wa Ghana kwenda kuungana tena na kocha wake wa zamani Nasreddine Nabi, jambo ambalo tulifichua wiki kadhaa zilizopita.Nabi, ambaye hivi karibuni alichukua mikoba huko FAR Rabat baada ya kuachana na Mabingwa wa muda wote wa Ligi Kuu ya Tanzania, Young Africans SC, alipendekeza kwa dhati kusajiliwa kwa Morrison wakati wakijiandaa kwa msimu ujao.

Mchezaji huyo asiyeishiwa vituko ndani na nje ya uwanja, amepewa mkataba wa mwaka mmoja tu na mabingwa hao wa Morocco kama mchezaji huru baada ya kuondoka Young Africans mwishoni mwa msimu wa 2022-23 wakiendelea kumtazamaia mwenendo wa tabia yake.

Katika kipindi chake akiwa na Young Africans, Morrison alicheza mechi sita na alifunga mara moja katika michuano ya Kombe la Shirikisho la CAF, ambayo iliwapeleka fainali, ingawa walishindwa na USM Alger ya Algeria.

Morrison (30) ambaye aliwahi kucheza Yanga akaenda Simba kisha akarejea Yanga tena, msimu uliopita alichangia pakubwa katika kuisaidia timu yake kutetea taji la Ligi Kuu ya Tanzania na Kombe la Shirikisho la Azam.Kabla ya kujiunga na AS FAR Rabat, mchezaji huyo wa zamani wa Heart of Lion na AshantiGold SC za Ghana alikaribia kumalizana na Singida Fountain Gate ya Tanzania, lakini makubaliano hayo yalivurugika wakati wa mazungumzo.

Hapo awali, Morrison aliwahi kucheza katika klabu maarufu kama vile Orlando Pirates ya Afrika Kusini, AS Vita Club ya Kongo na Simba SC, ambao ni wapinzani wa Young Africans.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz