Simba yatolea ufafanuzi ajali aliyopata Che Malone - EDUSPORTSTZ

Latest

Simba yatolea ufafanuzi ajali aliyopata Che Malone

 Simba yatolea ufafanuzi ajali aliyopata Che Malone

Pata 50,000 BURE Kila Siku Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amethibitisha kuwa ni kweli beki wao Che Malone Fondo amepata ajali leo Septemba 25 alfajiri akiwa anatoka uwanja wa ndege kupokea ndugu zake waliokuwa wamekuja kumtembelea.


Ahmed amesema kuwa tayari mchezaji huyo ameshakamilisha taratibu za hospitali na polisi na sasa ameruhusiwa kwenda nyumbani kupumzika.


Hata hivyo amesema Beki wao hajaumia kabisa (yupo fiti) katika ajali Ile aliyeumia ni kaka yake ambaye alipata michubuko kidogo.


"Ni kweli Che Malone amepata ajali leo maeneo ya mikocheni na hadi sasa ameshamaliza taratibu zote za hospitali na polisi na amekwenda nyumbani kupumzika"


"Hakuwa ametoka kula bata kama wengine wanavyosema," Simba inatarajia kutoa taarifa rasmi ya ajari hiyo muda mcheche kuanzia sasa.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz